September 30, 2013





Pamoja na kwambna dalili zinaonyesha kasi ya Simba ni nzuri baada ya kuitungua JKT Ruvu mabao 2-0 katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, jana. Mshambuliaji wake, Amissi Tambwe ni noma.



Tambwe, raia wa Burundi, jana aliweka rekodi ya kufunga mabao saba katika mechi sita, kitu ambacho hakijafanywa na mchezaji mwingine katika siku za hivi karibuni.

Tambwe aliipatia timu yake bao la kwanza katika dakika ya 24 kwa njia ya penalti kufuatia Omary Mtaki wa JKT kuunawa mpira katika eneo la hatari.

Tambwe sasa amefikisha mabao saba na kujikita kileleni mwa chati ya ufungaji akiwazidi wanaomkaribia, Jerry Tegete, Didier Kavumbagu, Themi Felix na Haruna Chanongo kwa zaidi ya mabao matatu.

Bao lingine la Simba katika mchezo wa jana liliwekwa kimiani na Ramadhani Singano ‘Messi’ dakika ya 49, kazi kubwa ikifanywa na Abdulhalim Humud aliyewatoka mabeki wa JKT na kupiga krosi iliyotumiwa vizuri na Messi.

Katika mchezo huo, JKT Ruvu ndiyo iliyoshambuliwa zaidi. Mfano, katika dakika ya 55, kipa wa JKT, Shaaban Dihile alilazimika kuokoa faulo iliyopigwa na Messi ambayo angeiacha ingeweza kuzaa bao la tatu.

Kiungo mahiri wa Simba, Amri Kiemba jana soka lilimkataa baada ya kupoteza mipira mingi na kulazimika kutolewa dakika ya 28 tu, nafasi yake ikachukuliwa na Messi.

Kioja katika mchezo huo kilikuwa ni mwamuzi kumpa kadi ya njano Humud katika dakika ya 17 wakati aliyetakiwa kupewa ni Joseph Owino aliyemchezea vibaya Shabani Kondo.

Baada ya mchezo huo, baadhi ya wachezaji wa JKT walimzonga mwamuzi wakidai alikuwa akiwakandamiza na kuipendelea Simba.


Simba: Abel Dhaira, Haruna Shamte, Adeyun Seif, Joseph Owino, Gilbert Kaze, Humud, Amri Kiemba/Messi, Said Hamis, Tambwe, Betram Mombeki na Chanongo.

JKT Ruvu: Dihile, Damasi Makwaya, Stanley Nkomola, Omari Mtaki, Jamal Said, Nashoni Naftari, Alhaji Zege, Emmanuel Swita, Bakari Kondo, Salum Machaku na Emmanuel Pius.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic