Wanachama wa
Yanga wanaotaka kufanya maandamano wameamua kuandika barua kwa Waziri wa Mambo
ya Ndani, Emmanuel Nchimbi.
Habari za
uhakika kutoka kwa mmoja wa wanachama hao zinaeleza, wameamua kuandika barua ya
kuomba ruhusa ya kuandamana kupiga uonevu wanaofanyiwa na TFF.
“Kweli
tumemuandikia Waziri Nchimbi na imepokelewa ofisini kwake hata ushahidi tunao.
Tumeamua kufanya hivyo baada ya kuona Jeshi la Polisi Kanda ya Dar es Salaam
wanatuzungusha.
“Tuliomba
kibali cha maandamano, wao wakatupa kibali cha mkusanyiko. Tukawaeleza vizuri
tunachotaka wakawa wanatuzungusha ndiyo maana tumeona tuvuke hadi kwa waziri na
sasa tunasubiri,” alisema mwanachama huyo.
Kuhusiana
na suala hilo, uongozi wa Yanga umekuwa ukikataa kulizungumzia na kusema
wanachama ndiyo wanaohusika.
Wanachama
hao wanataka kufanya maandamano ya amani kupinga moja kwa moja suala wanalodai
ni uonevu wa TFF dhidi yao katika mambo mbalimbali.
Tayari TFF
imeishaonya kuhusiana na hilo, kwamba viongozi wanapaswa kulishughulikia suala
hilo kabla ya maandamano kufanyika.
0 COMMENTS:
Post a Comment