Neema imezidi kumnyookea kiungo mshambuliaji wa Al-Markhiya Spors
Club ya Qatar, Mwinyi Kazimoto baada ya kocha mkuu timu hiyo raia wa Misri kumpanga
dakika zote 90 katika mechi za timu hiyo
Kazimoto alijiunga na timu hiyo inayoshiriki Ligi Daraja la Pili
Qatar hivi karibuni akitokea Simba ya Dar es Salaam.
Akizungumza na Championi Ijumaa, mwakilishi wa timu hiyo Saleh
Afif alisema kuwa kiungo huyo hivi sasa ameanza kuaminika kwa kocha wake na
kupewa dakika 90 za kucheza kwenye mechi.
“Kazimoto alipojiunga na Al-Markhiya alikuwa anapangwa kucheza
kipindi kimoja pekee, lakini hivi sasa anacheza dakika zote tisini. Hiyo
imetokana na kocha wake kuamini uwezo wake, ni jambo la heri kwake katika
mafanikio na kuongeza bidii zaidi akiwa uwanjani.
“Mechi yake ya kwanza kucheza dakika 90 ni ya kirafiki dhidi ya Al
Arabi inayoshiriki Ligi Kuu ya Qatar na kufanikiwa kufunga bao kwa shuti kali
nje ya 18,” alisema Afif.
0 COMMENTS:
Post a Comment