CHEKA AKIMCHAKAZA MMAREKANI.. |
Bondia maarufu nchini, Francis Cheka amesema anatarajia kuanza masomo Jumatatu ya
keshokutwa lakini akaenda mbali zaidi kwa kusema kuwa miongoni mwa
vilivyomshawishi ni kuona vijana wenzake wengi wanatumia mtandao wa Facebook
wakati yeye akiwa hajui lolote.
Bingwa huyo wa Dunia wa IBF, amepata ofa ya kusoma bure katika
shule ya Sekondari ya Mt Joseph ya Morogoro amefunguka kuwa elimu yake ni ya
darasa la saba, hivyo kwa kuwa nafasi hiyo imejitokeza, yeye ataitumia
kujielimisha zaidi.
“Kila kitu tayari na nitaanza kuingia darasani Jumatatu. Nimeamua
kuchukua masomo yenye tija zaidi katika ulimwengu wa sasa, masomo ya biashara,
Kiingereza na Kompyuta.
“Huwa naumia nikiona washikaji zangu wanasema wanaingia Facebook,
nahamasika kujua nini maana ya Facebook, kwa kweli sijui maana yake, labda
pengine ni kutokana na lugha, ndiyo maana nikamua kujifunza Kiingereza pia,”
alisema Cheka.
0 COMMENTS:
Post a Comment