Baada ya
kurudi nchini akitokea India kufanyiwa upasuaji wa goti, kiungo wa Simba, Kiggi
Makasi, atalazimika kuwa nje ya uwanja kwa muda wa miezi mitatu ili kupona
majeraha yake.
Kiggi
alikwenda India, Septemba 9, mwaka huu kufanyiwa upasuaji wa goti aliloumia
kwenye mechi ya kirafiki dhidi ya CDA ya Dodoma mapema mwaka huu.
Daktari wa Simba, Yassin Gembe alisema: “Anaendelea vizuri
ambapo kwa mujibu wa madaktari wa India atatakiwa kupumzika kwa muda wa miezi
mitatu kisha ndiyo ataanza mazoezi mepesi.”
Aidha, taarifa
kutoka ndani ya klabu hiyo zinaeleza kuwa, gharama zote alizotumia mchezaji
huyo akiwa India kwa matibabu na mambo mengine ni shilingi milioni 15.








0 COMMENTS:
Post a Comment