Beki wa
zamani wa Yanga, Shadrack Nsajigwa ambaye alikuwa kocha mkuu wa Lipuli FC ya
Iringa, ameamua kuachana rasmi na timu hiyo inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza
Tanzania Bara ikiwa ni siku chache tangu aanze kibarua hicho.
Nsajigwa amefikia uamuzi huo wa haraka kutokana na mazingira
magumu ya ufundishaji aliyokuwa akikutana nayo huku uongozi wake ukionekana
kutojali.
Inaelezwa kuwa Nsajigwa hakutimiziwa
mahitaji ya mechi ambayo alihitaji ili kurahisisha kazi yake ya ufundishaji
lakini akawa hatekelezewi.
“Wiki iliyopita alirejea Dar akitokea
Iringa baada ya kupata matatizo ya kifamilia, kipindi hicho anaaga alikuwa
tayari ameshamwambia mmiliki wa timu hiyo kuwa amechoshwa na maisha ya hapa,
hivyo aliomba kuondoka mwenyewe.
“Alipofika Dar kuna jamaa yake
akamtaarifu kuwa ni bora asirejee Iringa kwa kuwa baadhi ya viongozi waliweka
mikakati ya kumchafua katika mechi dhidi ya Kimondo itakayochezwa kesho
Jumamosi,” alisema mtoa habari wetu.
Alipoulizwa Nsajigwa kuhusiana na
taarifa hizo alisema: “Ni kweli nimeachana na timu hiyo, hivi sasa ninavyozungumza
na wewe nipo Dar ninafanya mambo yangu
binafsi.”








0 COMMENTS:
Post a Comment