September 24, 2013


Kocha Mkuu wa Azam FC, Stewart Hall amewataka wachezaji wake nyota kubadilika mara moja la sivyo ataendelea kuwatumia makinda.


Katika mechi dhidi ya Yanga, kikosi kilianza bila ya nyota Salum Abubakari ‘Sure Boy’ na Kipre Tchetche aliyeingia baadaye.

Hall raia wa Uingereza amesema wachezaji wake wengi wamekuwa hawawajibiki hali iliyomfanya alazimike kuwaacha katika mechi iliyopita dhidi ya Yanga.

“Nimewaleza kuhusiana na hili na kama hakutakuwa na aliyeelewa, basi sitatoa nafasi kwao.

“Tunacheza kwa ajili ya timu lakini sasa inaonekana kuna baadhi wamejisahau na wanajiona ni nyota sana,” alisema.

“Siwezi kuwa na matabaka katika kikosi, ninachotaka kila mmoja acheze kwa ajili ya timu si yeye binafsi.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic