MESSI AKIPAMBANA NA BAENA, HII ILIKUWA MISIMU ULIOPITA |
Kiungo wa Rayo Vallecano, Raúl Baena amemlaumu mshambuliaji Leo Messi wa Barcelona kwamba ndiye alikuwa chanzo cha wao kutosalimiana.
Baena alituhumiwa na vyombo vya habari kwamba hakumpa mkono Messi wakati timu zao zilipokutana katika mechi ya La Liga lakini yeye amesema Messi ndiye hakumpa mkono yeye.
"Inawezekana aliyeripoti suala hilo alishindwa kufanya kazi yake vizuri lakini sisi tulikuwa wenyeji na wenyewe ndiye wanatembea kutupa mikono.
“Lakini alipofika kwangu Leo hakunipa mkono na utaona nilikuwa nimeinua ili kumsalimia. Lakini sioni tatizo kama vipi tunaweza kukutana na kulirekebisha suala hilo,” alisema Baena.
Suala la wachezaji hao kutopeana mkono limezua gumzo na kuwagawanya wapenda soka katika makundi mawili, moja likimtetea Messi na jingine likimuandama Baena.
0 COMMENTS:
Post a Comment