Man United Vs Bayer Leverkusen
Man United chini ya David Moyes, wameishinda Bayer
Leverkusen kwa mabao 4-2.
Man United walionekana kutawala zaidi mchezo huo
wakiwa nyumbani na walifanikiwa kufunga mabao yao kupitia Wayne Rooney (dk ya
22 na 70) na van Persie katika dakika ya 5 na Valencia akapachika la nne.
Hata hivyo, wageni hao walifanya mambo kuwa si
lahisi kwa Man United kwa kufunga mabao mawili kupitia kwa Simon Rolfes na Omer
Toprak na kufanya matokeo yawe 4-2.
Wageni walijitutumua lakini bado ilionekana uzoefu wa
Man United ulikuwa unawasaidia zaidi wenyeji hao.
Galatasaray Vs Real Madrid
Pamoja na kuwa ugenini, Madrid imefanikiwa kuichapa
Galatasaray nyumbani kwao kwa mabao 6-1.
Kikosi cha Carlo Ancelotti kilitawala zaidi mchezo
huo na kupata bao moja katika kipindi cha kwanza lililofungwa na Isco katika
dakika ya 33.
Mshambuliaji wao nyota, Didier Drogba alitolewa nje
mapema baada ya kuumia.
Angelo Di Maria alitoa pasi ya pili ya bao baada ya
ile ya kwanza, safari hii akimpa Karim Benzema aliyefunga bao la pili kabla ya
Ronaldo kufunga la tatu katika dakika ya 63 na dakika tatu baadaye akafunga la
nne.
Dakika ya 81, Benzema akaongeza la tano kabla ya
Galatasaray kupata la kufutia machozi katika dakika ya 84 kupitia Bulut.
Dakika ya 90, Ronaldo akakamilisha adhabu kwa
wenyeji wao kwa kufunga bao la sita naye akiwa amepiga Hat trick.
Bayern Vs CSKA
Mabingwa watetezi wakiwa nyumbani waliiburuza CSKA
na kuonyesha hawataki mchezo katika kutetea taji.
Bayern waliibuka na ushindi wa 3-0 na walipata mabao
yao kupitia David Alaba, Mandzukic na Arjen Robben.
Plzen Vs Man City
Pamoja na kuwa ugenini, Man City safari hii
walionyesha wamepania kufanya mabadiliko ligi ya mabingwa kwa kushinda kwa
mabao 3-0.
Mabao ya Edin Dzeko, Yaya Toure na Sergio Aguero
walifanya usiku wa Kocha Manuel Pellegrini kuwa raha mustarehe.
MATOKEO MENGINE:
Benfica 2 Vs Anderlecht 0
Olympiakos 1 Vs PSG 4
FC Copenhagen 1 Vs Juventus 1
Real Sociedad 0 Vs Shaktar Donetsk 2
Man United Vs Bayer Leverkusen
0 COMMENTS:
Post a Comment