Mshambuliaji
wa zamani wa Manchester United, Teddy Sheringham ameibuka na mapya baada ya
kusema klabu hiyo imekosea kumsajili Marouane Fellaini.
Sheringham
amesema kocha David Moyes angemsajili kiungo mshambuliaji Mesut Ozil aliyesajiliwa na Arsenal kwa dau
kubwa la pauni milioni 42.5.
Mshambuliaji
huyo wa zamania amesema Ozil angekuwa na msaada mkubwa kwa Man United kuliko
Fellaini.
Mkongwe
huyo aliyewahi kuipa Man United ubingwa wa England, Kombe la FA na Ligi ya
Mabingwa, amesema Ozil angekuwa na msaada mkubwa zaidi kwa Man United.
“Naona
kama Ozil angekuwa na msaada mkubwa na utaona mechi yake ya kwanza aliyoichezea
Arsenal, alikuwa na msaada mkubwa. Lakini Fellaini ni mchezaji ambaye hana tofauti
kubwa na anavyocheza Michael Carrick,” alisem.
Kauli hiyo ya Sheringham huenda ikaanzisha mjadala mpya na
kumuweka Fellaini katika hali ya wasiwasi ingawa kwa mtindo wa Man United, bado
ana nafasi ya kufanya vizuri.
0 COMMENTS:
Post a Comment