September 21, 2013





Kikosi cha Mbeya City kimedhihirisha kwamba si lelemama baada ya kupata sare nyingine na kigogo, Simba.


Mbeya City imetoka sare ya mabao 2-2 na Simba katika mechi ya Ligi kuu ya Vodacom kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar, leo.
Mabao yote ya Simba yalifungwa na Mrundi Amissi Tambwe kabla ya Mbeya City kusawazisha kupitia Paul Nonga na Richard Peter katika dakika ya 68.
Mechi ilikuwa kali na ya kuvutia na mashabiki walishangilia kuanzia mwanzo hadi mwisho.
Mbeya City inayofundishwa na Juma Mwambusi imepanda Ligi Kuu Bara msimu huu.
Wiki iliyopita ilipata sare na bao 1-1 na mabingwa watetezi Yanga katika mechi iliyochezwa mjini Mbeya na kutawaliwa na vurugu.
Mechi nyingine ya ligi hiyo, Ashanti United imeendelea kugawa pointi baada ya kutwangwa mabao 3-0 na Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic