Kasi ya Leo Messi kwa msimu huu inaonekana kubwa zaidi kuliko wakati mwingine wowote.
Kabla ya mechi ya leo dhidi ya Vallecas, Messi anaonyesha ana kiwango kizuri zaidi kulikoa alivyoanza misimu mingine ya La Liga na Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Angalia hapa;Messi amefunga mabao sita katika mechi tatu tu za La Liga, halafu akaenda kuongeza mengine matatu katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, Jumatano.
Maana yake katika mechi nne, amefunga mabao tisa na hiyo ni kasi ya kimbunga.
Muargentina huyo amefikisha mechi 250 za La Liga na ameishafunga mabao 221, hiyo ni rekodi nyingine ya aina yake.








0 COMMENTS:
Post a Comment