Kocha Jose Mourinho wa Chelsea amemtaka
Andre Villas-Boas wa Tottenham kumheshimu na kuachana na maneno mengi.
Mourinho raia wa Ureno kama ilivyo kwa
AVB amesema amemfundisha mambo mengi kocha huyo anayopaswa kujivunia sasa.
Amesema anashangazwa na maneno mengi
anayotoa AVB aliyekwua msaidizi wake akiwa Chelsea na amesahau mengi aliyomfundisha
yanayomfanya aonekane moja ya makocha wazuri.
Amesema alikuwa akimfudisha kila
kilicho sahihi wakati wakifanya kazi wote na anatakiwa kuonyesha shukurani
badala ya maneno mengi yanayoonyesha kumvunjia heshima.
Mourinho
ndiye alimchukua AVB akaajiliwa Chelsea katika kitengo cha kusaka vipaji
kuanzia 2004 hadi 2009 yeye alipohamia Inter Milan.
Hivi
karibuni AVB amekuwa akisukuma maneno yanayoonyesha wazi kumshambulia Mourinho.









0 COMMENTS:
Post a Comment