![]() |
| MATA AKIWA MAZOEZINI NA WENZAKE.. |
Kiungo Juan Mata amesema hana kinyongo wala hofu na atacheza namba atakayopangwa na kocha wake Jose Mourinho.
Mata amesema atacheza kama namba kumi au winga kutegemeana na kocha wake anataka vipi.
Kumekuwa na gumzo kubwa kuhusiana na Mata aliyejiunga na Chelsea kwa dau la pauni milioni 25 akitokea Valencia.
Gumzo linatokana na uamuzi wa Mourinho kuamua kumtuliza benchi katika mechi za Premiership.
Lakini Mourinho aliamua kumchezesha katika mechi ya Capital One Cup na inaonekana kuna maelewano kati yao ndio maana amezungumzia suala hilo.
Mata ni kati ya wachezaji bora zaidi Chelsea kwa mujibu wa takwimu tokea msimu uliopita.
KATIKA MSIMU WAKE WA KWANZA;
- Mata alitengeneza nafasi 197 kwa Chelsea. Aliyemfuatia alikuwa ni Frank Lampard akiwa na 86.
- Alifunga mabao 18 ya ligi, Lampard akashika nafasi ya pili akiwa na 26.
- Alitoa pasi 25 zilizozaa mabao.
- Amepiga pasi 3,324 kama mchezaji wa Chelsea.
- Mata amepiga krosi 201, nyingi kuliko alizopiga yoyote.








0 COMMENTS:
Post a Comment