![]() |
| HOLLAND AKIWA NA MOURINHO KATIKA BENCHI LA CHELSEA.. |
Msaidizi wa Kocha José Mourinho
aitwaye Steve Holland amesema mshambuliaji wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo
alibadilika na kuwa wa kiwango cha juu zaidi alipokuwa akifanya kazi na kocha
huyo.
Holland ambaye sasa ni msaidizi wa
Mourinho katika kikosi cha Chelsea amesema kocha huyo Mreno amefanya kazi kubwa
kumbadili Ronaldo.
“Utaona namna alivyobadilika katika
kipindi cha miaka mitatu iliyopita na kuwa tishio, Mourinho anajua namna ya
kumbadilisha mchezaji.
“Amemfundisha Ronaldo mambo mengi ya
msingi ambayo hakika yalimbadili na kumfanya awe tishio duniani, anapaswa
kumshukuru Mourinho katika hilo,” alisema Holland.
Mourinho alifanya kazi na Ronaldo wakati wakiwa Real Madrid na sasa ametua Chelsea ambayo aliwahi kuifundisha kabla.








0 COMMENTS:
Post a Comment