![]() |
| VISA (KULIA) AKIWA KAZINI |
Hata hivyo,
Wakenya wengiw amepinga kutumia mitandao wakitaka mchezaji raga huyo, Visa
Oshwal aachiwe huru.
Oshwal
alijitokeza kuwa kati ya watu waliokuwa wakisaidia walioumia kutokana na tukio
la kigaidi katika jumpa la biashara la Westland jijini Nairobi.
Lakini
ghafla, askari wa usalama wakamkamata wakihofu huenda alikuwa gaidi
aliyejikausha na alitaka kuwakwepa kwa kutumia kigezo cha kusaidia.
Habari zimeeleza
kumatwa kwa Oshwal kulitokana naye kutokuwa amevaa beji ya Red Cross, hali
iliyowatia mashabiki baadhi ya polisi waliokuwa eneo hilo.
Asilimia kubwa
ya magaidi wameelezwa kutoroka kama raia wema, hali ambayo imewafanya askari
kuwa makini zaidi ndani na nje ya jengo hilo.
Lakini Wakenya
wengi kupitia mitandao mbalimbali wamekuwa wakieleza kuwa wanamtambua vizuri Oshwal
kama mchezaji mahiri wa raga.
Pamoja na
hivyo wamesisitiza polisi imuachie kwa kuwa ni mtu mwema ambaye kamwe hakuwahi
kuguswa au kuhusishwa hata na ugomvi wa mtaani.
Bado haijaelezwa
kama Jeshi la Polisi la Kenya limeishamuachia Oshwal ambaye hata alipokamatwa
alisisitiza alifika pale kwa ajili ya kusaidia.
Magaidi wa
Al Shaabab wameua watu takribani 70 katika shambulizi la kushitukiza katika
jumla hilo la biashara jijini Nairobi.








0 COMMENTS:
Post a Comment