Sakata la kiungo
Mrisho Ngassa limechukua sura mpya baada ya kupata ofa ya Sh milioni 105.
Awali Ngassa alikuwa
tayari kusaini mkataba mdogo wa maelewano na klabu ya Yanga ili alipiwe deni la
Sh milioni 45 kwa Simba, naye atakuwa akikatwa Sh 500,000 kila mwezi katika
mshahara wake.
Lakini sasa Ngassa
ametaka apewe siku kadhaa na kutafakari kuhusiana na suala la ofa hiyo kutoka
Oman.
Pamoja na uamuzi wake
wa kutafakari, bado inaonekana Ngassa anabanwa na mkataba wa Yanga ambao ndiyo
wenye haki naye baada ya TFF kumpitisha upande wa Jangwani na si Msimbazi.
Hivyo, hata kama
akiamua kuondoka, atalazimika kuomba ruhusa ya Yanga ambao kama hawataki,
atakuwa ‘ameumia’.
Habari kutoka ndani
ya Yanga zimeeleza, suala hilo linashughulikiwa na lilianza kufanyiwa kazi
tokea kwenye mkutano na chakula cha usiku kilichoongozwa na mwenyekiti wa
Yanga, Yusuf Manji.
Blog hii ilikuwa ya
kwanza kuandika jana kuhusiana mkutano huo kwenye hoteli ya Serena.
Ngassa alionyesha
kiwango kizuri akiwa na Simba msimu uliopita, kwani katika 27 alizocheza, 6
akiwa ameingia na 7 ametoka, alifanikiwa kufunga mabao saba na pasi 15 zenye
macho zilizozaa mabao.
Ngassa ataungana na
wenzake rasmi kesho kwa ajili ya kambi tayari kuivaa Ruvu Shooting Jumamosi na
atacheza uwapo tu Yanga watakubali kumlipia deni hilo.








0 COMMENTS:
Post a Comment