September 15, 2013

Mshambuliaji nyota wa Yanga, Mrisho Ngassa amesema ataendelea kujifua kwa nguvu na kikosi hicho bila ya kujali anacheza au la.

Ngassa yuko na kikosi cha Yanga mjini Mbeya na amekuwa akiendelea na mazoezi kama kawaida.

“Niko na wenzangu na mazoezi nayachukulia kama kitu makini, nafanya kwa juhudi kama kesho nitacheza.

“Najua kama nikifanya kwa juhudi maana yake nitasaidia kupandisha morali ya wenzangu,” alisema.
NGASSA AKIWA NA WACHEZAJI WENZAKE WA YANGA KATIKA UWANJA WA SOKOINE MJINI MBEYA, LEO

Ngassa amefungiwa mechi sita na kutakiwa kuilipa Simba Sh milioni 45 badala ya 30 alizokuwa amechukua Simba baada ya kusaini mkataba.




Nyota huyo amekuwa akiendelea na mazoezini na kikosi hicho cha Yanga ambacho kinaivaa Prisons, Jumatano mjini humo.


Awali katika mechi yake ya kwanza mjini humo, Yanga ilitoka sare ya bao 1-1 na Mbeya City katika mechi iliyotawaliwa na vurugu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic