Nigeria imefanikiwa kusonga katika hatua ya mwisho kuwania
kucheza Kombe la Dunia baada ya kuwafunga wageni wake Malawi kwa mabao 2-0.
Mabao ya Nigeria ‘The Super Eagles; yamefungwa na Emmanuel
Eminike katika dakika ya 44 na mshambuliaji Victor Moses wa Chelsea ambaye
amekwenda Everton kwa mkopo akafunga la pili katika dakika za mwisho kwa mkwaju
wa penalty.
The Flames walikuwa wamepania kushinda mechi hiyo iliyochezewa
dakika chache zilizopita kwenye Uwanja
wa UJ Esuene mjini Calabar, Nigeria
Nigeria ilitawala kipindi cha kwanza kuanzia katika na ikafanya
hivyo mara tu baada ya kuanza kwa kipindi cha pili huku kiungo wa Chelsea, John
Mikel Obi akitawala dimba.
Hivi karibuni, Kocha Mkuu wa Malawi, Tom Saintfiet aliyewahi
kuifundisha Yanga ya Tanzania aliingia katika mgogoro mkubwa na kocha wa
Nigeria, Stefen Keshi ambaye alimuita mpuuzi kwa kulaani mechi hiyo kupelekwa
kwenye mji wa Calabar.
Beki Limbikani Mzava wa Malawi alitolewa kwa kadi nyekundu baada
ya kumuangusha Ahmed Musa na Moses akafunga mkwaju huo.
Droo ya kupanga timu zitakazocheza katika hatua ya mwisho
itafanyika Septemba 16 jijini Cairo, Misri.
0 COMMENTS:
Post a Comment