Timu ya Mbeya City ya jijini hapa, imekabidhiwa
fedha taslimu Sh milioni moja baada ya kufanikiwa kuibana Yanga kwa kuilazimisha
sare ya bao 1-1.
Aliyetoa mkwanja huo ni Mbunge wa Jimbo
la Songwa mkoani hapa, Philipo Mulugo ambaye pia ni Naibu Waziri wa Elimu na
Mafunzo ya Ufundi. Mulugo ni mdau mkubwa wa soka mkoani hapa.
Mbeya, juzi ilitoka sare ya kufungana
bao 1-1 na Yanga kwenye mchezo uliopigwa katika Uwanja wa Sokoine jijini hapa.
Mulugo alisema aliahidi kuipa timu hiyo Sh milioni mbili kama
ingeibuka na ushindi lakini kwa kuwa ilitoka sare, ametoa Sh milioni moja.
“Si matokeo mabaya, ni matokeo safi,
lakini niliahidi kama wangeshinda basi ningewapa mbili ila kwa kuwa wamedroo
basi nimewapa moja kama pongezi kwao kwa mchezo mzuri waliouonyesha,” alisema
Mulugo.
Fedha hizo alikabidhiwa kocha mkuu wa
timu hiyo, Juma Mwambusi.








0 COMMENTS:
Post a Comment