Pamoja na kuwa na
wachezaji wake wote nyota, Real Madrid imeonja kipigo cha kwanza cha La Liga.
Madrid imefungwa 1-0
na wapinzani wake wakubwa Atletico Madrid tena ikiwa kwenye uwanja wa nyumbani
wa Santiago Bernabeu.
Bao hilo pekee
lililoacha majonzik na kipigo cha kwanza kwa kikosi cha Carlo Ancelotti
lilifungwa na Diego Costa katika dakika ya 11.
Kutokana na ushindi huo, Atletico Madrid iliendelea kubaki nafasi ya pili ikiwa na pointi 21 sawa na vinara Barcelona wakati Madrid inabaki nafasi ya tatu.
Katika kipindi cha
pili Madrid walishambulia mfululizo lakini mwisho wakaambulia kipigo hicho
kutoka kwa watani wao hao wa jadi wanaonolewa na Diego Simione, kiungo wa
zamani wa nyota Argentina.
Real
Madrid Diego Lopez, Arbeloa, Ramos, Pepe, Coentrao, Illaramendi,
(Modric 45) Di Maria (Bale 45), Isco, Ronaldo, Benzema (Morata 73).
Subs Casillas, Carvajal,
Casemiro, Varane
Atletico
Madrid Courtois, Juanfran, Miranda, Godin, Filipe Luis, Koke,
Tiago, Gabi, Arda Turan, Diego Costa, Villa
Subs Aranzubia,
Alderweireld, Guilavogui, Rodriguez, Oliver, Garcia, Baptistao







0 COMMENTS:
Post a Comment