Beki Mtanzania, Shomari Kapombe wa AS Cannes, ameongezewa muda wa
mapumziko hadi mwezi ujao.
Kitengo cha afya cha klabu hiyo, kimetangaza kuwa Kapombe ambaye
alifanyiwa upasuaji wa kidole, analazimika kusubiri zaidi kabla ya kuanza
mazoezi.
“Atakuwa nje zaidi hadi Oktoba, tutaangalia afya yake na baada ya hapo
tutaeleza ataanza lini mazoezi,” alisema Pierre ambaye ni mmoja wa wahusika wa
kitengo hicho, alipozungumza na Championi Ijumaa, jana.
“Baada ya kufanyiwa upasuaji, tuliona hakuwa amepona vizuri hata baada
ya zile siku tulizoamini zinatosha. Hivyo tumempa siku zaidi lakini kama
nilivyosema matarajio ni hadi Oktoba.”
Awali AS Cannes inayoshiriki Ligi Daraja la Nne nchini Ufaransa,
ilitangaza Kapombe atakuwa nje ya uwanja kwa siku 15 kutokana na kufanyiwa
upasuaji wa kidole ambacho kilikuwa kinamsumbua na ikafikia hadi akashindwa
kuvaa viatu.








0 COMMENTS:
Post a Comment