Simba ndiyo timu iliyoweka rekodi kwa
msimu wa pili mfululizo kuwa na kikosi kinachoshiriki Ligi Kuu Bara chenye
vijana wengi zaidi.
Msimu uliopita, Simba ilitumia wachezaji
wake makinda wengi kuliko timu nyingine. Awali mashabiki wengi walilalamika
sana lakini baadaye wakabadilika na kuwaunga mkono wachezaji wao.
Timu iliishia katika nafasi ya tatu huku
ikivuliwa ubingwa na watani wake wa jadi Yanga, lakini bado ikawa imejenga
msingi wa vijana.
Pamoja na uongozi kuamua msimu kusajili
wakongwe kadhaa ili kuunda kikosi imara, lakini bado Simba inaendelea kuwa na
vijana wengi zaidi katika kikosi chake kinachoshiriki ligi kuu.
Picha hii inaweza kuwa mfano mzuri, kwani
hili ndilo benchi la Simba wakati ilipocheza jana dhidi ya KMKM ya Zanzibar
kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar.
Katika mechi hiyo ya kirafiki, wachezaji
wengi vijana walikuwa katika benchi kama wanavyoonekana hapa katika picha,
kwani kati ya wachezaji wote mkongwe ni Betram Mombeki na waliobaki, wengi ni
chini ya miaka 20.
Huenda ni mfumo mzuri ambao umeanzishwa
na Simba lakini itakuwa vizuri zaidi vijana hao pia wakapewa nafasi ya kucheza
kwa kuwa msimu uliopita walionyesha uwezo mkubwa na kuwa wanaweza kucheza
katika kikosi cha kwanza na kufanya vizuri.
0 COMMENTS:
Post a Comment