Mrundi Amissi Tambwe ameonyesha anayeahidi anastahili kutumiza baada ya kufunga mabao mawili mengine katika mechi ya Simba dhidi ya Mbeya City inayoendelea kwenye Uwanja wa Taifa, Dar.
Tambwe alitoa ahadi ya kuendelea kupachika mabao mara baada ya kufunga mabao manne katika mechi dhidi ya Mgambo ambayo Simba ilishinda 6-0.
Baada ya mechi hiyo, Tambwe aliiambia Salehjembe kwamba ataendelea kupachika mabao kwa kuwa ameanza kuizoea ligi kuu.
Tayari Mrundi huyo alikuwa ameifungia Simba mabao mawili katika mechi dhidi ya Mbeya City na Msimbazi walikuwa wanaongoa kwa mabao 2-1.
BAo la Mbeya City limetupiwa kimiani na mshambuliaji mwingine hatari nchini, Paul Nonga.
0 COMMENTS:
Post a Comment