Klabu ya Simba imesema imeshtukia hujuma
na fujo zinazoandaliwa na watanai wao wa jadi Yanga wakati timu yao ikivaana na
Mbeya City katika mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara.
Akizungumza jijini Dar es Salaam Ofisa
Habari wa timu hiyo, Ezekiel Kamwaga alisema kuwa wamepata taarifa za mashabiki
wa Yanga kupanga kuvaa jezi za Simba zenye rangi ya nyekundu na nyeupe kwa
ajili ya kulipa kisasi kwa Mbeya City.
Kamwaga, ameliomba Shirikisho la Soka
Tanzania (TFF) kwa ajili ya kushirikiana na jeshi la polisi kulinda usalama
kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
“Tumepata taarifa za watani wetu wa jadi
Yanga kupanga kulipa kisasi cha kuwafanyia fujo wapinzani wetu Mbeya katika
mechi ya kesho.
“Wamepanga kuvaa jezi zetu zenye rangi
nyekundu na nyeupe kama njia ya kuonekana mashabiki wa Simba wakati siyo,
tunaiomba TFF kwa kushirikiana na jeshi la polisi kumchukulia hatua kali
shabiki yeyote wa Simba atakayefanya fujo ili iwe fundisho kwa wengine,”
alisema Kamwaga.
Yanga katika mechi yao dhidi ya Mbeya
City walifanyiwa fujo mbalimbali ikiwemo basi lao kuvunjwa vioo wengine
wakinusurika kupigwa.
0 COMMENTS:
Post a Comment