Baraza la Wazee wa Klabu ya Yanga,
umekanusha kwa nguvu zote taarifa za kuwa na mgogoro na uongozi wa klabu hiyo.
Tamko hilo, limetolewa leo mchana na
katibu wa baraza hilo, Ibrahim Akilimali ambaye amesema hakuna ukweli wowote
juu ya taarifa za kuwepo kwa ugomvi kati ya wazee hao na uongozi wa klabu hiyo.
Akilimali, maarufu kama Abramovich,
amesema baraza lake lina imani kubwa na uongozi wa juu wa klabu hiyo,
unaongozwa na Yusuf Manji, na kusema kasi ya ushindi wa timu yao ulioianza
dhidi ya Ruvu Shooting wikiendi iliyopita, ndio kazi imeanza ambapo yoyote
atakayekatiza mbele atapokea kichapo.
“Hakuna ugomvi kabisa sisi ndiyo
tumewakabidhi madaraka hawa vijana wetu, inawezekana watu walichanganywa na
hali ilivyokuwa hapa kati, yote yaliyotokea ilikuwa ni katika kujenga na siyo
kubomoa, sisi wazee tunasema ni sawa na maharage kuwa yanachemka na kurukaruka
katika sufuria ndiyo yanavyoiva vizuri,” alisema Akilimali aliyeongozana na
wenzake na mwenyekiti wake, Mzee Jabir Katundu.
Mara kadhaa, Akilimali amekuwa
akisisitiza kwamba hawana mgogoro na uongozi wa klabu hiyo.
Hisia kwamba kuna msigano zilitokana
nauamuzi wa Akilimali na wazee wenzake kumtimua Mkenya, Patrick Naggi
aliyekwenda klabuni hapo na kujitambulisha ni katibu mkuu mpya.
0 COMMENTS:
Post a Comment