KIFUKWE AKIZUNGUMZA... |
Uongozi wa Yanga, umesema bado upo
makini na mpango wao wa ujenzi wa Uwanja wa kisasa wa klabu hiyo, lakini
ukaiitaja serikali imesababisha kutokana na ukimya wake.
Akizungumza na Waandishi wa habari leo jijini
Dar es Salaam, Mwenyekiti wa mradi huo wa ujenzi wa Yanga, Francis Kifukwe amesema mpaka sasa
kilichokwamisha kuanza kwa ujenzi huo, ni eneo la ziada wanalolihitaji kiasi
cha hekta 10, litakalotosheleza katika mpango huo.
Kifukwe, ambaye ni mwenyekiti wa zamani
wa klabu hiyo, amesema tayari wameshaiandikia barua mbili serikali kupitia wizara ya Ardhi na Makazi,
zenye kumbukumbu namba YASC /ARDHI/MWK/YM/46/2012 na YASC/ARDHI/MWK/YM/47/2012,
kutaka kuomba eneo hilo la ziada ambapo mpaka sasa barua hizo hazijajibiwa.
“Jibu tunalolipata kutoka serikalini ni
kwamba bado wanazifanyia kazi, lakini kama haitoshi tena mwaka huu mwezi wa
saba, uongozi wetu ulimwandikia barua Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,
kuomba msaada wake kufanikisha maombi ya nyongeza ya kiwanja yaliyowasilishwa
Manispaa ya Ilala na Wizara ya Ardhi, sasa tunasubiri jibu lake,” alisema
Kifukwe.
SEHEMU YA NJANO NDIYO WANAYOMILIKI YANGA, ILIYO NA RANGI YA BLUU NDIYO WAMEOMBA SERIKALINI NA WAKO TAYARI KULIPA FIDIA KATIKA NYUMBA ZILIZO KATIKA ENEO HILO |
Aidha, Kifukwe amesema kuwa endapo
serikali itawakubalia kuwapatia eneo hilo, Yanga itajenga majengo mengi
mbalimbali ya kisasa mbali na Uwanja utakaokuwa na uwezo wa kuchukua watu
40,000, zikiwemo kumbi za kisasa za mikutano maduka,Supermarket, Sinema na sehemu za kubarizi, ambapo yote hayo
yakikamilika eneo hilo litabadilishwa jina na kuitwa ‘Jangwani City.’
BAADHI YA WAZEE WAKISILIZA LEO |
Hata hivyo, Kifukwe ambaye pia yupo
katika Baraza la Wadhamini la Yanga, amesema hata kama serikali haitawakubalia
maombi yao mradi huo hautakufa na badala yake watakutana na kampuni ya Wachina
ya BCEG, kuangalia nini wanaweza kujenga kwa eneo la hekta 3.59 linalomilikiwa
na klabu hiyo.
0 COMMENTS:
Post a Comment