September 20, 2013




Mshambuliaji wa Simba, Haroun Chanongo alifanikiwa kuifungia timu yake mabao mawili katika ushindi wa mabao 6-0 dhidi ya Mgambo, juzi lakini moja kati ya mabao hayo, yalionyesha kumkera bosi wa Yanga, Seif Ahmeid ‘Seif Magari’ na kulazimika kuondoka uwanjani.


Katika mechi hiyo kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar, gazeti hili lilimshuhudia Seif akiwa uwanjani hapo kuanzia mwanzo mpaka mwanzoni mwa kipindi cha pili, ambapo wakati huo Simba ilikuwa mbele kwa mabao 4-0.

Wakati kipindi cha pili kikiendelea, ilipofika dakika ya 64 Chanongo aliwakimbiza mabeki wa Mgambo na kuachia shuti kali lililojaa moja kwa moja wavuni, likiwa ni bao la tano kwa Simba na la pili kwake, ndipo hapohapo Seif akaamua kuinua na kutokomea zake nje ya uwanja.

Haikujulikana mara moja juu ya sababu ya Seif ambaye ni mema wa bodi ya Wadhamini wa Yanga kuondoka uwanjani hapo.

Hata hivyo, Seif hakuweza kulizungumzia suala hilo baada ya kuwahi kuondoka uwanjani hapo na simu yake kuita bila ya kupokelewa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic