September 15, 2013



Uongozi wa klabu ya Yanga umesema unataka mchezo kati yao na Mbeya City urudiwe katika uwanja huru.

Uamuzi huo unatokana na vurugu zilizotokea katika mechi ya jana dhidi ya timu hizo mbili.


Basi la Yanga lilipasuliwa vioo na kusababisha dereva wao kujeruhiwa.

Mashabiki wa Mbeya City walilishambulia kwa mawe na kusababisha hali hiyo.

Mjumbe wa Sekretarieti ya Yanga, Patrick Naggi raia wa Kenya alisema wana ushahidi kutokana na yaliyotokea.

“Kila kitu kipo na vurugu zilizofanyika hazikuwa za kiuanamichezo kabisa, zimechangia kwa kiasi kikubwa kuingiza hofu katika timu yetu,” alisema Naggi, kocha mwenye leseni ya Caf.
Msemaji wa Yanga, Baraka Kizuguto alilalamika kwa uongozi wa Chama cha Soka Mbeya kilikuwa kikiwakwepa kuhusiana na mpangilio mzima wa suala la ulinzi.

Mechi hiyo ya Ligi Kuu Bara ilimalizika kwa sare ya bao 1-1 na kuwa sare ya pili mfululizo kwa Yanga.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic