Bondia
Mayweather ameendeleza rekodi ya kucheza
mapambano 46 bila ya kupoteza hata moja huku akiwa ameshinda 26 kwa KO.
Mayweather ambaye aliingia ulingoni akisindikizwa na rafiki
yake Li Wayne alionyesha uwezo mkubwa ingawa mpinzani wake hakuwa laini.
Leo asubuhi, Mayweather amefanikiwa kumshinda Saul Alvarez wa
Mexico ambaye kabla alikuwa hajapoteza pambano hata moja.
Jaji wa kwanza alitoa sare ya pointi 114-114, lakini wawili wakatoa ushindi kwa Mayweather kwa pointi 116-112, 117-111.
Mayweather alitawala karibia raundi zote kuanzia ya tatu
akipiga ngumi moja moja za kudokoa ambazo zilimzidi Mmexico huyo.
Alvarez alionyesha uwezo kwa kupambana hadi mwisho, hata
hivyo Mayweather alionyesha ni bora zaidi yake kiufundi.
Namna alivyokuwa anakwepa na kupiga, alimpa wakati mgumu
Alvarez ambaye pia alionyesha atakuwa tishio zaidi.
Hilo lilikuwa ni pambano la kwanza la Alvarez kupoteza baada
ya kucheza mapambano zaidi ya 40, huku Mayweather akiendelea na rekodi ya
kutopoteza.
0 COMMENTS:
Post a Comment