Mjini Magharibi imetwaa ubingwa wa michuano ya Copa Coca-Cola kwa
vijana wenye umri chini ya miaka 15 upande wa wavulana baada ya jana (Septemba
14 mwaka huu) kuifunga Ilala bao 1-0.
Mechi hiyo ya fainali ilichezwa Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume
jijini Dar es Salaam. Ilala iliwavua ubingwa Morogoro baada ya kuwafunga kwenye
mechi ya nusu fainali kwa kuivua ubingwa Morogoro katika mechi iliyoamriwa kwa
mikwaju ya penalti.
Kwa upande wa wasichana, Mwanza ndiyo imeibuka na ushindi wa mabao
2-0 kwa njia ya penalti dhidi ya Ilala. Hadi muda wa kawaida wa mchezo huo
uliochezwa jana (Septemba 14 mwaka huu) jioni Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume,
jijini Dar es Salaam timu hizo zilikuwa suluhu.








0 COMMENTS:
Post a Comment