Aliyekuwa mgombea wa Urais wa
TFF, Richard Julius Rukambura aliyefungiwa miaka 20 na Kamati
ya Rufani ya Maadili ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), amesema atakwenda
mahakama kuu kutengua uamuzi huo.
Rukambura amesema amefikia uamuzi huo kwenda mahakama
kuu ili kupata haki yake huku akisisitiza, hana nia ya kusimamisha uchaguzi
mkuu wa TFF.
“Nakwenda mahakama kuu kwenda kupata haki yangu, sina
maana nitaenda kuiomba mahakama itengue uamuzi huo ambao si sahihi,” alisema na
alipoulizwa kuwa haoni si sahihi kwa mambo ya mpira kupelekwa mahakamani,
alisema.
“Lazima ujue sheria za Fifa si sheria za Tanzania, hivi
ni vitu ambavyo vinapishana lakini kama Mtanzania nina haki yangu na
inawezekana kuipata hapo.”
Sekretarieti ya TFF iliwasilisha
maombi ya mapitio kwa Kamati ya Rufani ya Maadili ili kupata mwongozo kwa vile
kulikuwapo mkanganyiko kwenye uamuzi wa Kamati ya Maadili, hivyo kuiwia vigumu
kwake kuutekeleza.
Uamuzi huo wa mapitio umesomwa leo
jioni (Oktoba 15 mwaka huu) mbele ya waandishi wa habari na wajumbe wa Kamati
hiyo wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti Victoria Makani.
Rukambura amefungiwa miaka 20
baada ya kupeleka masuala ya mpira wa miguu katika mahakama za kawaida kinyume
na Ibara ya 75 ya Katiba ya TFF na kifungu cha 73(3)(b) cha Kanuni za Maadili
za TFF toleo la 2013. Adhabu yake itamalizika Oktoba 15, 2033.
0 COMMENTS:
Post a Comment