Vijana wa kizungu wamefunga barabara
mjini Newcastle huku wakiimba nyimbo za kuwasifia ndugu wawili, Yaya na Kolo
Toure.
Vijana hao wa Kiingereza walifanya
hivyo na kusababisha foleni iliyodumu kwa dakika 10 huku madereva wakionyesha
kukasirishwa nao na kuanza kupiga honi wakitaka wapishwe.
Ajabu zaidi ni kwamba, mashabiki hao
walikuwa na furaha kubwa kwa kuwa England ilifanikiwa kufuzu kucheza Kombe la
Dunia nchini Brazil.
Lakini kijana mmoja mwenye mapenzi na
Yaya ndiye alianza kuimba na baadaye kundi kubwa la vijana waliokuwa wamelewa
wakaungana naye.
0 COMMENTS:
Post a Comment