Azam imefanikiwa kujiongezea pointi tatu
muhimu baada ya kuichapa Mgambo Shooting kwa mabao 2-0.
Katika mechi
hiyo ya Ligi Kuu ya Vodacom iliyochezwa kwenye Uwanja wa Chamazi jijini Dar, leo. Timu hizo zilikwenda
mapumziko zikiwa sare ya 0-0.
Kipindi cha
pili mambo yalibadilika na kupitia kwa Farid Malik aliyeingia kuchukua nafasi
ya Mganda, Bryan Umonyi.
Dakika ya
85, Kipre Herman Ttchetche akaifungia Azam Fc bao la pili kwa mkwaju wa
penalti.
Kwa ushindi
huo Azam FC imechuka hadi nafasi ya pili ikiwa na pointi 14 nyuma ya vinara
Simba wenye 15 na kufuatiwa na Yanga na JKT zenye 12 kila moja.
Hata hivyo,
Azam FC ina mchezo zaidi baada ya kucheza nane wakati timu nyingine zina mechi
saba.
0 COMMENTS:
Post a Comment