October 9, 2013





Kocha Mkuu wa Simba, Abdallah Kibadeni amesema hakuna nafasi kwa wachezaji wavivu.

Kibadeni amewataka wachezaji wa Simba kujituma huku akisisitiza, hakutakuwa na nafasi ya mchezaji asiyejituma kwa kisingizio cha jina au vinginevyo.


“Kila mtu lazima ajitume na nimekuwa nikiwaeleza, kama mtu anaona anajulikana hapa kwangu hakutakuwa na nafasi.

“Suala jingine la muhimu ni nidhamu, kazi yoyote na hata maisha kwa ujumla yanahitaji nidhamu,” alisema Kibadeni.

Yeye na kikosi chake wamejichimbia katika eneo la Bamba Beach, Kigamboni nje kidogo ya jiji la Dar.

Simba inayoongoza ligi inashuka tena dimbani Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar kuikaribisha Prisons ya Mbeya.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic