Kipa Ally Mustappha ‘Barthez’, beki
Nadir Haroub ‘Cannavaro’ wameachwa wakae jukwaani katika mechi ya leo dhidi ya
Rhino kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar.
Habari za uhakika kutoka ndani ya
Yanga zinaeleza wawili hao watakaa jukwaani, wakati Athumani Iddi ‘Chuji’ na
Didier Kavumbagu watakuwa benchi.
“Kweli tokea jana wanajua na kocha
ameamua kufanya hivyo, hatujajua sababu hasa nini nini lakini Kavumbagu alikuwa
amjeruhi ingawa ameishapona,” kilieleza chanzo.
Kocha Mkuu wa Yanga, Ernie Brandts
alikataa kuzungumzia suala hilo na kusema linaihusu timu yake na huu si wakati
mwafaka kulizungumzia.
0 COMMENTS:
Post a Comment