Wakati zoezi la kuhesabu kura linaendelea, taarifa zinaeleza
Jamal Malinzi ndiye Rais mpya wa Shirikisho la Soka Tanzania TFF.
Hali hiyo inatokana na kawaida ya uchaguzi inavyokuwa kwamba
wajumbe waliokuwa katika kambi ya Malinzi kama Wilfred Kidau, Geofrey Nyange ‘Kaburu’
na wengine wameshinda.
Dakika chache zilizopita, Mbunge wa Kigoma Kasikazini Zitto ame twitt naye akimpongeza Malinzi kwa ushindi.
Dakika chache zilizopita, Mbunge wa Kigoma Kasikazini Zitto ame twitt naye akimpongeza Malinzi kwa ushindi.
Katika uchaguzi wa TFF imekuwa ni kawaida kwa hali hiyo
kutokea kwamba wajumbe wengi wa kambi moja wakishinda, basi ndiyo aliyekuwa
upande wao akigombea urais anaibuka na ushindi.
Taarifa kutoka ndani ya chumba cha upigaji kura zinaeleza
wengi wao wamempigia kura Malinzi hali iliyofanya Nyamlani asome alama za
nyakati na kuamua kuondoka ukumbini.
0 COMMENTS:
Post a Comment