October 27, 2013


WAPIGA KURA WAKIWA KATIKA CHUMBA CHA MKUTANO LEO

Uchaguzi unaendelea katika Ukumbi wa Water Front jijini Dar.
Lakini vituko vimetawala na wagombea wamekuwa wakilalama kutokana na maandalizi ya kikao hicho.
Saa 8:31 Sherehe zinaanza, Malinzi ndiye mshindi na Tenga anazungumza akiahidi ushirikiano 
Saa 8:21 Kura zinamaliza kuhesabiwa na kila kitu safi, Malinzi ndiye Rais mpya wa TFF 
Saa 8:13 Mambo yamebadilika na Malinzi anaongoza kwa mbali
Saa 8:05 Kura zinaanza kuhesabiwa na Nyamlani anaongoza, upande wake wanaonekana kuwa na furaha
Saa 7:44 Kura za Rais zinaanza kuhesabiwa na dalili kuwa Malinzi atashinda 
Saa 7:25 Mshindi wa makamu wa rais anatangazwa ni Wallace Karia aliyewabwaga Nassib Ramadhani na Imani Madega 
Saa 6:38 Inaelezwa karibu kura za Rais zinaanza kuhesabiwa.
Saa 6:17 Kazi ya kuhesamu kura upande wa makamu inaendelea
Saa 5:58 Kura za makamu zinaanza kuhesabiwa, wagombea ni Wallace Karia, Imani Madega na Nassib Ramadhani.
Saa 5:45 Msafiri Mgoyi ameshinda kanda ya Tabora/Kigoma

Saa 5:25 Inajulikana Davis Mosha ameshindwa upande wa ujumbe kwa mikoa ya Tanga na Kilimanjaro
Saa 5:10 Kazi ya kuhesabu kura za wajumbe inaendelea
Wilfred Kidau ameshinda kanda ya Dar es Salaam.

Saa 4:30 Kazi ya kuhesabu kura za wajumbe inaendelea

Saa 3:58 Taarifa kutoka ndani ya chumba cha upigaji kura zinaeleza Geofrey Nyange 'Kaburu' ameshinda ujumbe kupitia Pwani.
Saa 3:46 Kura za Kanda ya 5 ndiyo zinahesabiwa
Saa 3:32 Madega na Wallace Karia wametangaza kuhesabu kura zao wenyewe

Saa 3:21 Mgombea wa Urais, Athumani Nyamlani anatoka katika chumba cha kura na kushuka chini, anaingia kwenye gari na kuondoka, wapambe wake wanataka kujua hali ikoje. Huyo anaondoka zake

 Saa 2:36 Kazi ya kuhesabu kura inaanza
 Saa 1:35 Upigaji kura wa upande wa makamu na baadaye rais umeanza, wajumbe wanaitwa kwa majina na kwenda kupiga
 Saa 1:29 usiku Mmiliki wa blogu, Jackson Odoyo anakamtwa akiwa amejificha katika katika chumba cha wapiga kura, anapigwa pingu na kwenda kupelekwa mahabusu kituo cha kati
Saa 12:24 Mchana Kura zinaendelea kupigwa na mambo ni siri sana
 Saa 11:42 Upigaji kura za wajumbe umemalizika na unaanza wa klabu
 Saa 11:07 Kazi ya upigaji kura inaanza 
 Saa 10:48 Wagombea wote wanapokonywa simu, kidogo inaonyesha kuwashitua

  Saa 10:30 Inagundulika zoezi halijaanza na watu wanatakiwa kuvuta subira
 Saa 10:00 Wajumbe wako kwenye ukumbi wa mkutano, taarifa za kuanza kwa kupiga kura.e
 Saa 9:00 Alasiri Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo (Taswa), Juma Pinto anawaambia waandishi kugomea kuripoti uchaguzi kutokana na TFF kuonyesha dharau waziwazi dhidi yao. Waandishi wengine wanaanza kuondoka eneo la tukio.
 Saa 7:45 Hali hiyo inatokana na uamuzi wa TFF kuwaondoa katika sehemu husika waliyokuwa wamekaa na wanataka kuwatoa
Saa 7:30 Lakini kuna mvutano mkubwa kati ya Polisi na Waandishi wa habari .
Saa 6:30 Mchana Kwa sasa ni mapumziko na wajumbe wakiwemo wagombea wamekwenda kupata chakula cha mchana.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic