Kocha wa zamani wa Man United, Alex
Ferguson amesema amekuwa karibu sana na Kocha, David Moyes.
Ferguson amesema amekuwa akishirikiana
na Moyes kwa kila kitu hasa kipindi ambacho kimekuwa kigumu kwake.
“Tunashirikiana na tumekuwa
tukizungumza sana katika siku za hivi karibuni.
“Najua kuna ugumu lakini itafikia mambo
yatabadilika na atafanya vizuri,” alisema.
Kuhusiana na kukaa nje ya soka,
Ferguson mwenye miaka 71, alisema:
“Nakumbuka vitu vingi sana kwa kweli,
nimezoea mapambano na pia mambo mengi ya soka.
“Lakini ukweli ni hivi, nimechukua
uamuzi sahihi katika wakati mwafaka, hivyo hakuna ninachojilaumu.”
0 COMMENTS:
Post a Comment