Beki Gerard Piqué wa Barcelona ametoa kauli ya kuwashangaza wengi baada ya kusema anavutiwa zaidi na mshambuliaji wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo.
"Cristiano ni mchapakazi na asilewa na mafanikio"
Habadiliki, ni mchezaji anayenivutia siku zote na mchapa kazi kila mchezo alio uwanjani. Ni mashine ya ukweli na hajaacha kutaka kuongeza kiwango chake kila siku.
"Tunabadili utawala wa Real Madrid"
Miaka yote, Barcelona imekuwa ikifuatia baada ya Real Madrid, ndani ya miaka 10 au 15, tumeleta mabadiliko makubwa na utaona ule utawala wa miaka kama 90 wa Real Madrid umekwisha.
"Tunachuana na mamilionea wa dunia"
Barcelona ni vijana, tumeanza kupanda taratibu na viongozi ndiyo mabadiliko. Real Madrid waliwahi kumaliza msimu bila kuchukua hata taji moja baada ya kutumia uero milioni 160 katika usajili wa wachezaji watatu tu (msimu uliopita). Angalia msimu huu, wamewasajili Illarramendi, Isco na Bale. Barcelona imemsajili Neymar tu tena kwa euro milioni 70 hivi, wengine wanatokea La Masia, utaona kiasi gani tunachuana na matajiri wa dunia.
"Pep ndiye kocha bora zaidi kwangu"
Unaweza kuniona tofauti lakini Pep Guardiola ndiye kocha bora zaidi kwangu katika niliowahi kufanya nao kazi. Alikuwa akitumia saa 24 kwa kuangalia CD mbalimbali za mechi za wapinzani au timu yetu inavyocheza. Utaona anarudisha nyuma, anapeleka mbele na siku inayofuata ana mafunzo
0 COMMENTS:
Post a Comment