Uongozi wa Simba umesema sasa hauna mjadala katika suala la fedha zao
wanazoidai klabu ya Etoile du Sahel ya Tunisia, badala yake watakwenda makao
makuu ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa).
Katibu Mkuu wa Simba, Evodius Mtawala amesema makubaliano ya mwisho
waliyofikia na Waarabu hao wa Tunisia ni kulipwa fedha zao dola 300,000 (Sh
milioni 480) na mwisho ilikuwa ni juzi.
“Lakini wameshindwa kutekeleza na Fifa wanajua tuliposaini makubaliano ya
awali kwamba mwisho watalipa ni Septemba 30, mwaka huu.
“Katikati ya Septemba tuliwakumbusha lakini wakawa kimya. Hivyo
tutakwenda Zurich ambako ni makao makuu ya Fifa ili kupata mwafaka wa suala
hilo,” alisema Mtawala.
Hivi karibuni, Etoile iliingia mgogoro na Okwi ambaye naye akasusa na
kuamua kurejea kwao Uganda na kujichimbia akidai hawajamlipa mshahara wa miezi
mitatu.
Baadaye alirejea jijini Dar na amekuwa akionekana akikatiza mitaa huku
akisisitiza yuko katika matembezi yake ya kawaida.
Simba ilifanya biashara ‘kichaa’ baada ya kumuuza Okwi halafu ikaondoka
Tunisia bila ya kuchukua hata senti ikisubiri ahadi ambayo imekuwa haitimizwi,
hadi leo.
0 COMMENTS:
Post a Comment