Zatlan Ibrahimovic ,32, amefunga bao la
aina yake kwa kisigino wakati PSG ilipoichapa Bastia kwa mabao 4-0 katika mechi
ya Ligi ya Ufaransa maarufu kama League 1.
Mswidi huyo alifunga mabao mawili
wakati Edinson Cavani akifunga moja katika ushindi huo mnono wa PSG ambayo
imetumia mamilioni ya fedha katika usajili wake.
AKIFUNGA BAO HILO |
Pamoja na ushindi huo, bao hilo la
kisigino limekuwa gumzo kutokana na namna alivyofunga akiwa katikati ya mabeki
wawili wa Bastia.
Ibra amekuwa akifunga mabao mazuri
kutokana na tabia yake ya kujiamini na amekuwa akisisitiza kwamba ana uwezo
mkubwa wa kucheza soka.
0 COMMENTS:
Post a Comment