Kama hakutakuwa na usamjo na wizi wa
kupindukia, mechi ya
kesho ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya
Simba na Yanga, huenda ikaweka rekodi ya mapato katika mechi yao ya leo.
Uwanja wa Taifa utakaotumika leo una uwezo wa kubeba takribani watu 60,000 tu na si zaidi.
Taarifa zilizoifikia blogu hii
zinaeleza hadi kufikia jana jioni, tiketi zote za mechi zilikuwa zimemalizika. Maana yake zimeuzwa kwa siku moja tu tena si zaidi ya saa 12.
Watu walianza kuzitafuta tiketi mapema
na vituo vingi vilikuwa vimefungwa, lakini baadaye zilianza kuuzwa.
Hadi kufikia saa 11, tiketi za Sh 5000
zilikuwa zimepotea kabisa na taarifa zikaelezwa kuwa zimeisha.
Baada ya hapo, watu walianza kununua
tiketi za karibu kila bei kutokana na kuhofia kukosa kabisa.
Baadhi ya viongozi wa Yanga na Simba
wamethibitisha kupata taarifa kwamba tiketi zimeuzwa zote.
Hii inashiria mambo mawili, kwanza
rekodi ya mauzo, lakini ulinzi lazima uwe imara kwa kuwa kama watu wataingizwa
kwa ujanja, kuna hofu ya uwanja kuzidiwa na watazamani, kitu ambacho ni hatari.
0 COMMENTS:
Post a Comment