Vibaka wenye roho mbaya wamemfanyia kitu mbaya msanii maarufu Mrisho Mpoto baada ya kuiba vitu mbalimbali katika gari lake.
Mpoto amesema ameibiwa vitu vya zaidi ya Sh milioni mbili baada ya vibaka hao kufanya uvamizi usiku wa manane.
‘Jamaa wamenitia hasara kubwa, naona wameitumia fursa vibaya na wamenirudisha nyumba kweli, nasikitika sana kwa kuwa walitaka kung’oa hadi viti.
“Lakini wameiba karibu kila kitu baada ya kuvunja vioo. Maana hadi pipe za AC nazo wameiba, ukiliona gari hauwezi,” alisema.
0 COMMENTS:
Post a Comment