October 25, 2013


Kisimbuzi kipya cha Azam TV kitakuwa na mwonekano tofauti kabisa na vingine.

TORRINGTON


Pamoja na hivyo, kisimbuzi hicho kilichoonyeshwa leo mbele ya waandishi wa habari, kitauzwa kwa bei lahisi zaidi huku kikiwa na chaneli takribani 50.

Kupitia Kisimbuzi hicho, Azam TV1 itakuwa ikionyesha moja kwa moja mechi za Ligi Kuu ya Tanzania Bara.

Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Azam Media, Ndugu Torrington amesema king’amuzi hicho kitalipiwa Sh 96,000 pamoja na gharama za ufungaji.
BAADHI YA WAFANYAKAZI WA AZAM TV


Halafu mtumiaji atalazimika kulipa Sh 12,500 tu kama malipo ya mwezi ambayo ni ya chini zaidi.

Alisisitiza kwamba wamefanya hivyo na hakuna makundi katika huduma zao, kwamba wengine ni tajiri na wengine ni masikini.

Huduma za king’amuzi hicho zinatarajia kuanza katikati ya mwezi ujao.

5 COMMENTS:

  1. Nahitaji receiver tu ya azam tv dish na kila kitu ninacho ila receiver yangu imeunguwa jana

    ReplyDelete
  2. Jinsi ya kupata kumbukumbu namba mm ni mteja mpya

    ReplyDelete
  3. Matangazo tumeyaona ila Arusha amjatuletea tatizo liko wapi?

    ReplyDelete
  4. Je kwa sasa kingamuzi kipya cha azam ni bei gani

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic