Kumekuwa na taarifa kwamba
huenda uchaguzi mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ukatawaliwa na
rushwa.
Uchaguzi huo umepangwa kufanyika keshokutwa Jumapili kwenye Ukumbi wa Water Front jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wajumbe wameeleza
kwamba kuna wagombea wametoa ahadi ya fedha kwa kila atakayewachagua.
Taarifa zinaeleza asilimia
kubwa ya wagombea wamekuwa wakipiga kampeni huku wakitanguliza fedha.
“Kila mgombea anaonyesha yuko
tayari kutoa fedha kwa wapiga kura, hii ni kuanzia ngazi za juu hadi chini.
“Tatizo ni moja tu, kuwa kila
upande wa mgombea unahofia uaminifu wa wapiga kura, kwamba wanaweza wakapokea
fedha halafu wasitimize ahadi wanapoingia kwenye kupiga kura,” alisema mmoja wa
wajumbe ambaye atapiga kura.
Kutokana na hali hiyo, simu
ndiyo zinaonekana kuwa nyenzo muhimu katika suala hilo.
“Kweli, kila mgombea anasema
hivi, atatoa fedha baada ya uchaguzi, na kitakachotumika kuhakikisha kama
umempigia kura au la ni simu.
“Yaani baada ya kupiga kura,
unatakiwa kuipiga picha ile karatasi yako ya kura kwa kutumia simu halafu
ukitoka unamuonyesha ili akupe fedha yako.
“Lakini wajumbe wengine wengi
nao hawataki hilo, wanataka kupewa kabla, sasa hapo kidogo kumekuwa na
kutoelewana.”
Uchunguzi wa Salehjembe,
unaonyesha kumekuwa na harufu ya rushwa katika uchaguzi huo na kuna baadhi ya
wagombea wamekuwa wakiahidi kipoza jasho kwa wapiga kura.
Mara kadhaa, uchaguzi maarufu
kama huo wa TFF umekuwa ukielezwa kutawaliwa na harufu ya rushwa, ingawa
haijahi kutokea mhusika kukamatwa.
0 COMMENTS:
Post a Comment