Kocha wa zamani wa Simba, Patrick Liewig
ametua nchini na kusema amekuja kuangalia mechi ya watani Jumapili, pamoja na
kudai fedha zake.
Liewig amesema hakumaliziwa fedha yake
na Simba ambao alikuwa anawadai zaidi ya dola 20,000, hivyo atajitahidi
kuwafikia ili wamalizane.
“Pamoja na hivyo nataka kuangalia mechi
na kuwaona vijana wangu, nataka kuwaona wachezaji niliowafundisha.
“Mfano Marcel (Kaheza), Chanongo, Ndemla
na wengine. Nasikia raha kwa kuwa ndiyo nilianza kuwapa nafasi,” alisema Liewig
ambaye tayari yuko jijini Dar es Salaam.
Kocha huyo aliifundisha Simba kwa nusu
msimu tu baada ya kuichukua kutoka mikononi mwa Mserbia, Milovan Cirkovic.
Wakati wa Liewig, Simba ilianza kutumia
vijana zaidi hali iliyosababisha baadhi ya wachezaji nyota kama Haruna Moshi ‘Boban’
na Juma Nyosso kuachwa.
0 COMMENTS:
Post a Comment