Baada ya Simba kuinyanyasa Yanga katika kampeni za NANI MTANI
JEMBE leo jijini Mwanza, Yanga wamelipa kisasi ndani ya A Town, yaani Arusha.
Katika mechi ya watani hao kwa timu za mashabiki iliyopigwa
kwenye Uwanja wa General Tyre jijini Arusha, Yanga imeibuka na ushindi wa bao
1-0.
Kabla jijini Mwanza maarufu kama Rock City, Yanga ilipoteza
kwa mabao 3-0, huku wengi wakiamini itarudisha zote, lakini wapi.
Bao la Yanga jijini Arusha lilifungwa na Elias Boti aliyepiga
shuti lililomshinda kipa wa Simba, Khatibu Ally na mwamuzi akasema “twendeni
kati”.
Pamoja na mchezo huo, huku watu wakiburudika na bia ya
Kilimanjaro, kazi ilikuwa ni kwenye kuvutana kwa kamba na kila upande
ulionyesha ubabe.
0 COMMENTS:
Post a Comment