Chelsea imeitandika
Manchester City kwa mabao 2-1 katika mechi ya Ligi Kuu England iliyocheza leo
jijini London.
Mechi hiyo ilikuwa kali na
ya kuvutia na Chelsea walikuwa wa kwanza kupata bao lao katika dakika ya 33 kupitia
Mjerumani Andre Schurrle aliyepokea krosi
safi ya Fernando Torres aliyewatoka mabeki wa Manchester City.
Lakini kupitia Kun Aguero,
Manchester City walisawazisha mara tu baada ya kupiga shuti kali ilikuwa katika
dakika ya 49.
Wakati ikionekana kama mechi
ilikuwa imemalizika, Torres alifunga bao baada ya kipa Joe Hart na mlinzi, Matija
Nastasic wa Manchester City kujichanganya wakati wakijitahidi kuokoa na Mhispania
huyo akawamaliza kwa ulaini.
Kocha wa Chelsea, Jose Mourinho alikuwa burudani zaidi mara baada ya Torres kufunga bao hilo muhimu.
Mourinho aliinuka na kwenda kushangilia kwa mashabiki utafikiri mshambuliaji aliyefunga bao.
0 COMMENTS:
Post a Comment