Moja ya burudani kali katika mechi
iliyopita ya Yanga na Simba, ilikuwa ni winga wa Simba, Mrisho Ngassa na beki wa
Yanga, David Luhende ambao walichuana vikali.
Luhende na Ngassa walichuana vikali kwa
kuwa wote wana sifa ya kuwa na kasi na uwezo mkubwa wa kumiliki mpira.
Lakini katika mechi ya leo, Ngassa na
Luhende wanaweza kucheza upande mmoja yaani 3 na 11 halafu wataunganisha mbio
zao kuwakimbiza Simba.
Kazi itakuwa kubwa, lakini Simba wana
wachezaji wanaoweza kuwazuia, nahodha Chollo na winga anaweza kuwa Kiemba au
Singano. Ila kazi ipo.
0 COMMENTS:
Post a Comment